RATIBA VPL YAREKEBISHWA, LIGI KUMALIZIKA APRILI 19
Bodi ya Ligi Kuu Tanzania (TPLB) imeifanyia marekebisho ratiba ya Ligi Kuu ya Vodacom (VPL) ambapo sasa itamalizika Aprili 19 mwaka huu badala ya Aprili 27 mwaka huu. Marekebisho hayo yamefanyika ili kutoa fursa kwa timu ya Taifa 9Taifa Stars) kujiandaa kwa mechi za mchujo la Kombe la Afrika 2015 ambapo itacheza raundi ya awali Mei mwaka huu. Kutokana na marekebisho hayo, Yanga itacheza na Prisons (Uwanja wa Taifa) Machi 26 mwaka huu katika mechi ya raundi ya 17 wakati Machi 19 mwaka huu kwenye uwanja huo huo ni Yanga na Azam. Machi 15 mwaka huu kutakuwa na mechi mbili; Azam na Coastal (Azam Complex), na Mtibwa Sugar itacheza na Yanga (Jamhuri). Mgambo na Azam zitacheza Machi 26 mwaka huu Mkwakwani, na Aprili 9 mwaka huu Yanga itaialika Kagera Sugar (Taifa). Raundi ya 22 itaanza Machi 22 mwaka huu kwa mechi kati ya Kagera vs Prisons (Kaitaba), JKT Ruvu vs Mbeya City (Azam Complex), na Rhino vs Yanga (Ali Hassan Mwinyi). Machi 23 mwaka huu ni…
Nenhum comentário:
Postar um comentário